Shirikisho la soka duniani FIFA limeahidi kutoa ushirikiano wa dhati
kwa baadhi ya vyombo vya habari, ambavyo vinaendelea kuibua taarifa za
hofu ya upangaji wa matokeo kwa baadhi ya timu ambazo zilifuzu kucheza
fainali za kombe la dunia mwaka huu.
Msemaji wa shirikisho hilo Rob Harris, amesema FIFA itaonyesha
ushirikiano kwa chombo chochote cha habari ambacho kitawasilisha
ushahidi wa kutosha, ambao utawashurutisha kuamini ni kweli kuna jambo
hilo ambalo linapigwa vita katika michezo.
Harris, amesema ni vigumu kwa sasa kutoa tamko lolote ama kuanza
kufanya uchuguzi kupitia taarifa ambazo zinaandikwa katika vyombo vya
habari vya nchini Uingereza pamoja na Ujerumani kwa kudai kuna harufu ya
mchezo mchafu wa upangaji wa matokeo.
Katika hatua nyingine msemaji huyo wa FIFA amesema mpaka sasa
hawajaona dalili zozote ambazo zinahusiana na mchezo mchafu wa upangaji
wa matokeo, hivyo wamevitaka vyombo vya habarti kuwa makini na taarifa
wanazozitoa kwenye jamii ya soka.
0 comments:
Post a Comment