Collabo ya Roma na Bob Junior iliyozaliwa kutokana na utani wa soka
imekuwa moja kati ya mada zilizozungumziwa jana huku mashabiki wakitoa
maoni tofauti kuhusu ngoma yao ya ‘Maumivu’.
Roma ameelezea jinsi anavyoichukulia
ngoma hiyo ambayo baadhi ya watu walionekana kumpinga kwa kufanya na Bob
Junior wanaesema hukata mauno.
“Nairank katika asilimia kubwa sana za juu though ina siku moja
tangu itoke kwa sababu officially tumeirelease jana. Na credit yangu
naitoa kwa sababu ya comments ambazo nazipata. Katika comments 44 nakuta
comments zinaonesha kuwa disappointed lakini zilizobaki zote zinakuwa
nzuri. Na hiyo nimeizoea tangu nimeanza muziki wangu. Sijawahi
kupokelewa positive tu. Watu wanashangaa hiyo collaboration jinsi
ilivyotokea na kusahau kwamba wapo wasanii wengi tu wa nyuma waliwahi
kufanya collabo na wasanii wa kuimba, Roma sio mtu wa kwanza.
“Nimeona hata jana katika mtando wa Facebook nikapata comments
kama 237 hivi, kati hizo comments ni comments 33 zimepinga lakini
zilizobakia zote wanasema muziki mzuri, ngoma kali na tumeielewa. Kwa
hiyo unaweza kuona hapo jinsi ambavyo watu wameipokea katika kiwango
kizuri.”
0 comments:
Post a Comment