Sunday, August 17, 2014

Yamoto Band wamtaja anaewaandikia nyimbo kwa asilimia 90



Yamoto Band wamtaja anaewaandikia nyimbo kwa asilimia 90Yamoto Band inayoundwa na wasanii wenye umri mdogo inazidi kufanya vizuri kila kukicha na hivi sasa wanatamba na ngoma tatu zikiwa ni pamoja na Nibemende/Nitajuta, Niseme.
Akiongea Jayree, Asley ambaye ni kiongozi wa bendi hiyo amesema kuwa Said Fella (boss wao) amekuwa msaaada mkubwa katika nyimbo zao zote.
“Mara nyingi sisi huwa tunafanya melodies yeye anatoa maneno…Producer alitengeneza beat akatuita studio tukaanza melodies na maneno kidogo yetu. Bahati nzuri Mkubwa alikuwa anatoka kwake anakuja studio tukampigia simu ‘mkubwa sisi tumepata melody kuna nyimbo tulikuwa tunafanya hapa studio ila bado tunaona maneno kama hayajakuwa mazuri. Kweli mkubwa alivyokuja kuyasikiliza akaanza kuyapasua neno maoja baada ya moja.”  Amesema Asley.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...