Kim Kardashian alionyesha umbo lake lenye mvuto kwenye tuzo za watu za GQ zilizofanyika jijini London, Jumanne usiku.
Kim Kardashian aliwashangaza watu wakati alipokwenda kwenye Tuzo za
GQ Watu wa Mwaka mjini London siku ya Jumanne usiku akiwa na gauni
lililobuniwa na Ralph na Russo lenye suti ya Atsuko Kudo na viatu virefu
vya Tom Ford.Akisindikizwa na mume wake Kanye West, ambaye hakuacha kumkumbatia, nyota huyo wa kipindi cha Keeping Up With The Kardashians alipewa tuzo ya Mwanamke wa Mwaka na mhariri wa GQ Dylan Jones.
Huzuni kwa Dylan, hakuweza kutaja jina lote lenye West mwishoni, na Kimmy alihakikisha kila mmoja analijua hilo (jina).

Kanye
West 37, akimsaidia mkewe kuweka gauni lake vizuri asije akalikanyaga
wakati anatembea kwenye zulia jekundu kwenye sherehe za Tuzo za Watu wa
Mwaka za GQ zilizofanyika mjini London.
Dylan alimtambulisha nyota huyo wa televisheni kwa maneno yafuatayo:
“Ni mmoja wa wanawake maafuru duniani. Malkia wa mitandao ya kijamii na
malkia wa televisheni. Na tangu aoane na Kanye West mwezi Mei, amekuwa
sehemu ya wanandoa maarufu duniani. Ni maarufu kwa Cocoa Cola. Ni Kim
Kardashian.”Kim na Kanye walidhihirisha kuwa ni wapendanao bora kwa kila mmoja kwa mwenzake, hawakuacha kutabasamu na rapa huyo alikuwa akijisogeza kwenye shingo ya mke wake mzuri na kuzungusha mikono yake kwake. Pia alimpiga busu kuwa alipokwenda kwenye jukwaa kupokea tuzo yake.

Wanandoa hao walifunga ndoa mwezi Mei mjini Florence nchini Italia.
0 comments:
Post a Comment