MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUOMBA KAZI SERIKALINI KWA WALIOSOMA NJE YA NCHI, WALIOPOTEZA VYETI NA WENYE MAJINA TOFAUTI NA VYETI VYAO
Sekretarieti ya ajira katika kutekeleza majukumu yake ya uendeshaji wa mchakato wa ajira Serikalini imekuwa ikikabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la baadhi ya waombaji kazi kupoteza, kuibiwa, kuharibikiwa au kuunguliwa vyeti vya kitaaluma pamoja na vitambulisho vinginevyo. Kutokana na baadhi ya waombaji kazi kutokufahamu taratibu za kufuata pindi wanapopoteza vyeti vyao au wanapobadilisha majina huamua kuwasilisha nyaraka pungufu Sekretarieti ya Ajira jambo ambalo husababisha kukosa nafasi ya kuchaguliwa au kukosa fursa ya kufanya usaili kwa kutokuwa na nyaraka zinazohitajika.
Hali hii imekuwa ikisababisha malalamiko kutoka kwa waombaji kazi wakati wa uhakiki kutokana na baadhi yao kuwa na nyaraka ambazo hazikidhi vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa tangazo la nafasi ya kazi. Kasoro hizo zimechangia baadhi ya wadau kuitupia lawama Sekretarieti ya Ajira kuwa ina
upendeleo, kwa kutokuwaita kwenye usaili wale waliobainika mapema kutokuwa na sifa au kuwazuia kufanya usaili waombaji wasiokuwa na nyaraka halisi na halali ikiwemo vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya taaluma. Ili kuthibitisha alichowasilisha awali kwa kuwa wengi wao huwa na result slip, hati matokeo (partial transcript) barua za utambulisho wa upotevu wa vyeti kupitia polisi ambazo baadhi yake huwa zimeshapita muda wake.
Jambo hili limepelekea baadhi ya wahitimu kujikuta njia panda kwa kushindwa kufahamu hatua za kuchukua ama taratibu za kufuata ili kuweza kupata vyeti vingine au namna ya kufikisha taarifa kwa mamlaka husika ili kuweza kupata msaada ama huduma stahili pindi nyaraka hizo zitakapohitajika mahali fulani. Hivyo, Sekretarieti ya Ajira inapenda kuwafahamisha wadau wake hususani waombaji kazi Serikalini kwamba haipokei barua ya utambulisho kutoka polisi inayohusu kupoteza, kuungua, kuibiwa, utofauti wa majina kati ya cheti kimoja na kingine kutokana na baadhi yao kuzitumia vibaya.
WAHITIMU WALIOPOTEZA VYETI WAZINGATIE YAFUATAYO;-
WAOMBAJI WALIOSOMA NJE YA NCHI WAZINGATIE YAFUATAYO;-
Sekretarieti ya Ajira pia inawasisitiza waombaji kazi wote waliosoma
Nje ya Nchi iwe ni elimu ngazi ya Sekondari au Vyuo Vikuu kwamba mara tu
baada ya kumaliza mafunzo wahakikishe wanapeleka taarifa zao hasa Vyeti
vya taaluma kwenye mamlaka husika mapema ili kuhakikiwa taarifa zao na
kupewa barua zinazothibitisha kutambuliwa kwa Vyuo walivyosoma ambapo
mamlaka zenye dhamana ya kuhakiki taarifa hizo ni Tume ya Usimamizi wa
Vyuo Vikuu (TCU), Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Baraza la
Usimamizi wa Elimu ya Vyuo vya Ufundi (NACTE). Kwa kuwa mamlaka hizo
ndio zenye dhamana kuthibitisha ama kuwasilisha taarifa za mhusika za
kupotelewa na vyeti katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira kwa mujibu wa
taratibu za uendeshaji wa Mchakato wa Ajira Serikalini na sio mtu
aliyepotelewa kuwasilisha utambulisho wa matokeo ama nyaraka mbalimbali
zikiwemo za kitaaluma wakati anapoomba kazi.
WAOMBAJI WENYE MAJINA TOFAUTI KWENYE VYETI WAZINGATIE YAFUATAYO;-
Kutokana na baadhi ya wadau wetu kubadilisha majina yao kwa kutokupenda kuendelea kutumia majina ya utotoni, ya kinyumbani au kubadili dini, kuolewa na kutumia ubini wa mume au kurithi majina ya walezi hali ambayo imechangia wengi wao kuwa na majina tofauti kati ya cheti kimoja na kingine iwe cha kuzaliwa ama cha kitaaluma, Sekretarieti ya Ajira inawataka wale wote wenye tofauti ya majina katika vyeti vyao kufuata taratibu za kisheria kabla ya kuwasilisha maombi ya kazi Sekretarieti ya Ajira kwa kwenda mahakamani na kula kiapo kwa kamishna wa viapo au kwa Wakili ili waweze kupata (Deedpal) au (Affidavity) kwa mujibu wa sheria, na sio kubadili majina kienyeji hali ambayo inaweza kuwanyima haki zao wakati mwingine. Kwa kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kuthibitisha uhalali wa tofauti ya majina au majina yake yote kutambulika kisheria.
Mwisho waombaji kazi wote wenye matatizo ya Vyeti wanashauriwa kuzingatia na kufuata utaratibu ulioelekezwa mara tu baada ya kupata matatizo ili taarifa zao ziweze kufika mapema Sekretarieti ya Ajira na pia inaweza kuzuia uwezekano wa aliyeiba au kuviokota kuvitumia. Aidha, itawasaidia wakati wanapoomba kazi kuepuka usumbufu na gharama zisizokuwa na ulazima.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Barua pepe: katibu@ajira.go.tz, gcu@ajira.go.tz,
Tovuti; www.ajira.go.tz, S.L.P. 63100 Dar es Salaam.
Simu; 255-687624975
0 comments:
Post a Comment