Thursday, September 11, 2014

Matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii huwanyima watumiaji nafasi ya kuajiriwa, fahamu wanachofanya waajiri nchini

Matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii huwanyima watumiaji nafasi ya kuajiriwa, fahamu wanachofanya waajiri nchini Mitandao ya kijamii inazidi kupata nafasi sio tu kwa watu kujifurahisha bali imegeuka kuwa sehemu ya utambuzi wa tabia na wasifu halisi wa watumiaji pale wanapotafuta ajira katika vitengo maalum.
Hayo yamebainishwa na meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy i.
Mungy ameeleza kuwa yeye ni mmoja kati ya watu wenye makampuni binafsi wanaofanya kazi ya utambuzi wa sifa halisi za mtu anaemba nafasi ya ajira na hupelekewa tenda na waajiri wengi.
Amesema mitandao ya kijamii huwa sehemu mojawapo ya kumfahamu vizuri mtu anaeomba nafasi hiyo ambapo hupata nafasi ya kufahamu jinsi wanachoandika kwenye mitandao na wanavyochukuliwa na jamii katika comments zao.
Haya ni maelezo ya Mungy:
“Tatizo sio tu kuonekana wanatumia vibaya. Ubaya ni kwamba hawa watu wanaharibiwa kitu kinaitwa sifa za uajiri. Ngoja niseme ukweli…mimi nina kampuni yangu na nafanya kitu kinaitwa kujaribu kutafuta wasifu wa mtu. Kwa mfano Times Fm hapa wanataka presenter mwenye nidhamu kufanya kipindi cha watoto. Sasa boss wenu hapa atakuja ataniambia ‘Mungy nina interview za majina haya hapa. Nataka unipe wasifu wao. Hawa watu wana wasifa gani kwenye jamii.
“Nitakwenda. Nina software yangu nitabandika pale ‘MC Pilipili naomba maneno Kumi tu unayotumia kwenye mitandao ya kijamii. Nikiangalia picha ntaandika picha ambazo ni kinyume na watu wengi na zitakuja na comments ambazo watu wamezitoa wanakuonaje. Na ile itatengeneza summary kabisa ya mfano MC Pilipili hafai kufanya kipindi cha watoto wadogo…
“Kwa hiyo ukienda kutafuta kazi unashangaa kila siku wewe barua zako hazijibiwi! Kumbe watu wameshaangalia kila siku wewe unaandika ‘nakula bata Q bar saa nane za usiku’ kila siku! Sasa huyu mtu anafanya kazi saa ngapi.” 

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...