RAIS wa shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba
amefunguka kuwa shirikisho lao linajishughulisha na maslahi ya wasanii
wote wa filamu na si kutumia muda mwingi kwa ajili ya matamasha na
misiba hiyo si kazi yao.
“TAFF inadili issue muhimu hatuhangaiki na mbwembwe za kujinuisha na
misiba au matamasha, tunaangalia mustakabali wa Sanaa yetu, na tumefanya
lobbying kwa waheshimiwa Wabunge kwa mara ya kwanza tasnia ya filamu na
muziki itaongelewa katika katiba,”anasema Mwakifwamba.
Rais huyo
amedai kuwa shirikisho lao limekuwa mbele kupigania maslahi ya wasanii
wote pasipo ubinafsi wa kujitengenezea fedha kwa kutumia wasanii na
wanaonufaika ni wachache na kuichafua tasnia nzima na kuonekana haifai
ikiongoza kwa kashfa.
0 comments:
Post a Comment