Mwanadada kutoka nchini Marekani Serena Jameka Williams
amefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya US Open upande wa wanawake
baada ya kumbanjua mpinzani wake kutoka nchini Denmark Caroline
Wozniacki.
Serena ambaye alikuwa akicheza katika viunga vya nyumbani alifanikisha suala la ushindi katika mchezo wa hatua ya fainali kwa kumshinda mpinzani wake kwa seti seti mbili bila majibu ambazo ni 6-3 na 6-3.
Ushindi huo unampa sifa nyingine mwanadada huyo kutoka nchini Marekani ya kutwaa ubingwa wa 18 wa michuano mikubwa ya mchezo wa Tennes *Gland Slams*
Mataji ya michuano mikubwa yaliyochukuliwa na Serena Williams mpaka sasa upande wa;
US Open (6): 1999, 2002, 2008, 2012, 2013 pamoja na 2014
Australian Open (5): 2003, 2005, 2007, 2009 pamoja na 2010
French Open (2): 2002 pamoja na 2013
Wimbledon (5): 2002, 2003, 2009, 2010 pamoja na 2012
Hatua ya fainali upande wa wanaume ya michuano ya US Open itachezwa hii leo mjini New York kati ya Kei Nishikori kutoka nchini Japan dhidi ya Marin Čilić kutoka nchini Croatia.
Wanafainali hawa walifanikiwa kushinda michezo yao ya hatua ya nusu fainali kwa kuwabanjua magwiji wa mchezo wa Tennes kwa sasa ambapo upande wa Kei Nishikori alimshinda Novak Djokovic kutoka nchini Serbia, ili hali Marin Čilić alimshinda Roger Federer.

0 comments:
Post a Comment