Kocha Carlo Ancelotti amefuta kabisa ndoto za Cristiano Ronaldo kurudi
Manchester United baada ya kufichua kwamba staa huyo Mreno atazeekea
Real Madrid. Ronaldo ameonyesha kuwa mwanasoka bora kabisa duniani kwa
sasa katika kipindi cha miaka yake mitano klabuni Real Madrid tangu
alipojiunga na timu hiyo kwa ada ya uhamisho wa Pauni 80 milioni
akitokea Man United mwaka 2009. Mwaka huu kumekuwa na uvumi kwamba
huenda Mreno huyo akarudi Old Trafford mwakani, lakini Ancelotti
ameibuka na kudai kwamba Real Madrid inamhitaji mwanasoka huyo bora
kubaki kwenye kikosi chao. Kocha huyo amesema kila mtu anaweza
kubadilishwa au kutolewa, lakini Ronaldo kwa sasa ni mwanasoka bora
duniani na kumpoteza hilo litakuwa pigo kubwa kwa Real Madrid. Ancelotti
pia amesisitiza kuwa hilo haliwezi kutokea, Ronaldo ataendelea kubaki
Real Madrid kwa kipindi chote cha maisha yake kwenye mchezo huu.
Amewahakikishia mashabiki wa Real kwa asilimia 100 kwamba Ronaldo
atabaki Madrid msimu ujao na si kwenda Manchester United, kwani amesema
mchezaji huyo anafurahia kuwa Real na anapendwa na kila mtu hivyo
atamaliza maisha yake ya soka akiwa Real.
0 comments:
Post a Comment