Mwandishi Marti Perarnau ambaye alizunguka mwaka mzima na kocha kijana
Pep Guardiola kwa ajili ya kuandika kitabu cha msimu wake wa kwanza
akiwa na Bayern Munich amefichua kwamba kocha huyo anatazamia kuwa kazi
yake inayofuata itakuwa England. Kauli hiyo huenda ikazua vita kwa klabu
mbalimbali kubwa za England ambazo zitapenda huduma yake. Kwa sasa
Guardiola ana mkataba na Bayern Munich mpaka mwaka 2016 akiwa anatokea
Barcelona ambapo alijijengea jina kubwa kwa kutwaa mataji mawili ya
ubingwa wa Ulaya, mataji matatu ya La Liga, mawili ya Kombe la Mfalme,
mawili ya Super Cup, na mawili ya Klabu Bingwa ya Dunia. Manchester City
inapewa nafasi kubwa ya kumchukua Guardiola kutokana na urafiki wake
mkubwa na mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo, Txiki Begiristain, ambaye
alicheza naye Barcelona na pia aliwahi kushika nafasi hiyo ya ukurugenzi
wa ufundi Barcelona wakati Guardiola akiwa kocha. Hata hivyo, kwa
uamuzi wake wa kutaka kwenda England utaiweka Arsenal katika tahadhari
wakati huu bosi mtendaji wa timu hiyo, Ivan Gatzidis akikiri kwamba
kunahitajika umakini mkubwa kumpata kocha mbadala kuchukua nafasi ya
Arsene Wenger mwenye umri wa miaka 65.
0 comments:
Post a Comment