Waliokuwa wanandoa, Mariah Carey na mchekeshaji Nick Cannon wanaripotiwa kugombea mbwa wao nane wanaowachukulia kama marafiki.
Kwa mujbu wa gazeti la Sunday Express, ugonvi wa Mariah Carey na Nick
Cannon umehamia kwenye mbwa wao nane waliokuwa wanaishi nao huku kila
mmoja akitaka kuwa mmiliki na mwangalizi halali baada ya kuachana.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa wawili hao wamemaliza mgogoro wa £325 Million kwa makubaliano maalum.
Mariah na Nick Cannon walitengana mwezi Augus mwaka ikiwa ni miaka kadhaa tangu walipofunga ndoa mwaka 2008.
Hivi sasa Nick Cannon amejikita zaidi katika kazi yake huku akiendelea na kazi mpya ya kummeneji Amber Rose.
Inaelezwa kuwa hivi sasa Mariah Carey anaonekana kuwa kupitia kipindi
kigumu na kwamba amenyong’onyea baada ya kuachana na mumewe huyo.
0 comments:
Post a Comment