Thursday, June 26, 2014

luis arejea nyumbani pamoja na adhabu kupewa

Luis Suarez amerejea kwao Uruguay na kupokelewa kishujua mjini Monte Video licha ya adhabu kubwa zaidi kuwahi kutolewa na FIFA kuning’inia juu ya kichwa chake. Hapa chini ni muhtasari wa mikasa aliyowahi kuhusika nayo.

June 2014
Amefungiwa kujishughulisha na soka kwa miezi minne, pamoja na mechi tisa za kimataifa, kwa kumng’ata mlinzi wa Italia, Giorgio Chiellini
April 2013
Aliomba radhi kwa kumng’ata Branislav Ivanovic mlinzi wa Chelsea na akatumikia adhabu ya kufungiwa mechi 10.
Dec 2011
Alipigwa adhabu ya kufungiwa mechi nane na kupigwa faini ya pauni 40,000 kwa kumtusi kiubaguzi wa rangi mlinzi Patrice Evra wa Manchester United.
Nov 2010
Alipigwa adhabu ya kufungiwa mechi saba kwa kumng’ata begani Otman Bakkal wa PSV Eindhoven’s Otman Bakkal wakati akichezea Ajax
July 2010
Alishika mpira kwa mkono wakati ukiingia golini na kuwanyima Ghana ushindi kwenye mechi ya robo fainali. Asamoah Gyan akakosa penati na kuipatia Uruguay nafasi ya kushinda kwa mikwaju ya penati kuamua mshindi kuingia nusu fainali.

No comments:

Post a Comment