Saturday, June 28, 2014

Shisha yapigwa marufuku kenya

Uvutaji Shisha wapigwa marufuku Kenya, hubeba dawa za kulevya
Kenya imepiga marufuku uvutaji wa Shisha (Sheesha) kwa ladha 19 baada ya kugundua kuwa zinabeba madawa ya kulevya kama heroin, bangi na cocaine.
Amri hiyo imetangazwa na kuongezewa uthibisho na chombo kinachoshughulikia kampeni ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya, NACADA (National Campaign Against Drug Abuse) ambacho kilieleza kuwa kimefanyia majaribia ladha 100 za Sheesha wakiwa na ofisi ya wizara ya afya na wamegundua kuwa aina hizo 19 hubeba madawa ya kulevya.
Kati ya ladha zilizopigwa marufu ni Al Fakher strawberry flavor, Al Fakher orange flavor, Al Fakher two apples with mint flavour, Al Fakher vanilla flavour, Al Fakher two appeals flavor, Al Fakher guava flavor, Al Fakher orange with mint flavor, Al Fakher orange flavor na nyingine.

No comments:

Post a Comment